THE AMAZON COLLEGE (T) LTD
TEGETA CAMPUS
P.o.Box 55832, Contact: Office. 0766-097249/0657-373732 Director 0655-030050/ 0755-030050
DAR ES SALAAM-TANZANIA
FOMU YA MAELEZO YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UREMBO, MITINDO YA NYWELE NA UREMBO WA KUCHA ( MAKEUP , HAIR DRESSING AND MANICURE )
JINA LA MWOMBAJI/MWANAFUNZI…………………………………………….
The amazon college Tegeta campus ni chuo kilichosajiliwa na serikali chini ya mamlaka ya mafunzo ya ufundi(NACTVETA) kwaajili ya kutoa kozi mbalimbali kwa ngazi ya cheti.
Campus hii ya Tegeta imejipanga kuhakikisha inatoa mafunzo yenye ubora wa hali ya juu hususani katika fani ya urembo,mitindo ya nywele na urembo wa kucha ( make up,hair dressing and manicure (nails beuty )
Hii ni fani yenye fursa nyingi za ajira hapa nchini katika miji mikubwa hata ile midogo inayakuwa hivyo ni fani inayotoa ajira nyingi sana hapa nchini. Tunavifaa na walimu mahili wenye kiu ya kufundisha mwanafunzi hadi aelewe.
The Amazon College inakualika kujiunga na chuo chetu katika kozi ya Urembo, mitindo ya nywele na urembo wa kucha (makeup,hair dressing and manicure ( nails beauty)
MAZINGIRA YA CHUO.
Chuo chetu kipo kwenye mazingira tulivu, madarasa makubwa yenye mwanga na hewa safi. Ni mazingira bora ya kujifunzia. Tunao walimu wenye taaluma ya kutosha kumuelisha na wenye kiu ya mafakio ya wanafunzi wao.
Faida ya kujiunga na kozi ya Urembo,mitindo ya nywele na urembo wa kucha(makeup,hair dressing and manicure (nails beauty )
- AJIRA ya UHAKIKA: Wahitimu wetu wamekuwa wakifanya vizuri katika soko la AJIRA hivyo kuacha sifa nzuri kila wanapoajiriwa katika maeneo mbalimbali.
- Utafundishwa na walimu mahiri na wenye kipaji na uzoefu wa kufundisha wanaozingatia taaluma ya ufundishaji.
- Sekta hii ni pana sana hivyo kupitia maarifa na ujuzi atakaopata chuoni mhitimu anauwezo wa kuamua kuajiriwa au kujiajiri.
- Kupitia fani hii mhitimu anaweza kujiajiri kwa kufungua saloon za kuremba na na kubuni mitindo mbalimbali ya nywele.
- Baada ya kumaliza mafunzo kwa Nadharia na vitendo na kufaulu mitihani yake kwa kupata alama nzuri mhitimu atakaye tunukiwa cheti ni yule aliyesoma kozi ya urembo au mitindo ya nywele tu (makeup or hair dressing).
MAKEUP,HAIR DRESSING AND NAILS BEAUTYMIHULA YA MASOMO KWA MWAKA 2023
MUHULA WA 1 | MUHULA WA 2 | MUHULA WA 3 | MUHULA WA 4 | MUHULA WA 5 |
07 NOV,2022 | 09 JAN,2023 | 13 MARCH,2023 | 08 MAY,2023 | 03 JULY,2023 |
Muda wa kozi na Gharama zake.
NO | KOZI | MUDA WA KOZI | ADA |
1 | FULL MAKEUP,HAIR DRESSING AND MANICURES | WIKI KUMI NA MBILI (12) | TZS 550,000/= |
2 | MAKEUP | WIKI SITA (6) | TZS 280,000/= |
3 | HAIR DRESSING | WIKI SITA (6) | TZS 280,000/= |
4 | MANICURE (NAILS BEAUTY) | WIKI TATU (3) | TZS 100,000/= |
Utasoma nadharia na vitendo
Sahihi ya mwanafunzi: _______________________ |
UTARATIBU WA KULIPA ADA.
Kozi ya Urembo,(Tzs 280,000)
- Ilipwe yote kabla ya kuanza masomoTzs 280,000/=
Kozi ya Mitindo ya nywele,(Tzs 280,000)
- Ilipwe yote kabla ya kuanza masomo Tzs 280,000/=
Kozi ya Urembo wa kucha,(Tzs 100,000)
- Ilipwe yote kabla ya kuanza masomo Tzs 100,000/=
Kozi ya Urembo,mitindo ya nywele na urembo wa kucha,(Tzs 550,000)
- Kabla ya kuanza masomo TZS 350,000/=
- Kabla ya kuanza mwezi wa pili wa masomo TZS 200,000/=
GHARAMA NYINGINE ZINAZOTAKIWA KULIPWA KABLA YA
MWANAFUNZI KUANZA MASOMO.
- Kitambulisho cha chuo 10,000/=
- T-shirt Tshs 15,000/=
- SARE (uniform) za chuo 60,000/=(Kwa wanafunzi watakaosoma full makeup, hair dressing and manicures)
Jumla ni shilingi 85,000/=
– Unifom zote zinapatikana chuoni.
SARE:
Wanafunzi wote wanavaa sare za chuo
MAHITAJI |
Suruali Nyeusi |
Shati jeupe la mikono mirefu |
kizibao cheusi |
Tai Nyeusi. (Wavulana) |
Skafu nyeusi (Wasichana) |
- Viatu vyeusi vinavyofunka mguu,Soksi nyeupe kwa wasichana na Soksi nyeusi kwa wavulana
MAHITAJI MUHIMU:
MAKEUP | HAIR DRESSING | MANICURE (NAILS BEAUTY) |
Daftari kubwa na kalamu ya blue | Daftari kubwa na kalamu ya blue | Daftari kubwa na kalamu ya blue |
Wanja,Consiller,Brash set na Foundation | Vibanio,Chanuo la mti,Mafuta | Buffer,Mkasi mdogo,Twizeer |
Powder,Banana powder,Eye shedol | Wiving,Raster,Spray malley |
SHERIA NA TARATIBU AMBAZO MWANAFUNZI UNAPASWA KUZINGATIA
- Kila mwanafunzi ni lazima awe na kitambulisho cha shule na avae shingoni muda wote, Ikiwa mwanafunzi amepoteza kitambulisho atapaswa kutoa taarifa kituo cha polisikisha alipie shuleni Tsh.10,000/= ili apatiwe kingine.
- Mwanafunzi unapaswa kuzingatia taratibu za uvaaji wa sare za chuo kama ulivyoelekezwa vinginevyo hutoruhusiwa kuingia darasani
- Wanafunzi wanaovaa hijabu, hawaruhusiwi kuvaaa hijabu za rangi nyingine tofauti na nyeupe
- Mwanafunzi haruhusiwi kuvaa kilemba au kofia kichwani, ikiwa unayo sababu maalum ya kufanya hivyo unapaswa kuomba kibali kwa mkuu wa chuo.
Sahihi ya mwanafunzi: _______________________ |
- Mwanafunzi haruhusiwi kutumia vileo mf. Pombe, uvutaji wa sigara au bangi n.k uwapo chuoni au katika mazingira ya chuo.Ukibainika utasimamishwa masomo moja kwa moja.
- Mwanafunzi hakikisha unahudhuria vipindi vyote vya darasani kila siku ya jumatatu mpaka ijumaa na unazingatia muda kwa kipindi chote cha masomo
- Mwanafunzi unapaswa kulipa ada kupitia benki kwa akaunti ya chuo utakayopewa na mhasibu hapa ofisini na si vinginevyo
- Mwanafunzi hakikisha unapewa risiti kwa malipo yote utakayofanya chuoni. Kama umefanya malipo na hukupewa risiti unawajibu wa kuidai.
- Mwanafunzi unapaswa kuzingatia utaratibu wa kulipa ada kidogo kidogo (kupunguza kila mwezi) kama ulivyoelekezwa ofisini.
- Mwanafunzi atakayeshindwa kulipa ada kwa utaratibu wa kupunguza kila mwezi uliowekwa na chuo atasimamishwa masomo mara moja.
- Mwanafunzi zingatia kutunza risiti zako za malipo ya ada ni muhimu mpaka utakapohitimu na kutunukiwa cheti.
- Mwanafunzi unapaswa kukamilisha malipo yako ya ada kabla ya kufanya mitihani yako ya mwisho.
- Ni lazima kila mwanafunzi afanye mazoezi yote atakayopewa na mwalimu darasani,pamoja na mitihani yote itakayotolewa na shule.
- Mahusiano ya kimapenzi kati yamwanafunzi na Mwanafunzi au mwanafunzi na mwalimu au na mfanyakazi yeyote wa shule ni marufuku kabisa
- Mwanafunzi atakayeghairisha masomo baada ya kulipa ada na kabla ya masomo kuanza atarudishiwa asilimia hamsini (50%) ya ada aliyolipa. (gharama za fomu ya kujiunga hazitarudishwa) Endapo utaamua kusitisha baada ya kuanza masomo ada haitarudishwa kwa namna yoyote.
- Ni lazima mwanafunzi atii na kufuata sheria zote zilizoorodheshwa hapo juu na zile nyingine utakazoendelea kupewa pindi awapo chuoni.
Baada ya kuhitimu hakikisha unachukua cheti chako mapema kabla ya kupita miezi miwili baada ya hapo kutakuwa na TOZO kwa kuchelewa kuchukua cheti.
Mimi ————————————————— nimesoma na kuelewa maelezo yaliyotolewa hapo juu na nimeamua kwa dhati kujiunga na masomo kwa kozi ya Urembo,mitindo ya nywele na urembo wa kucha(makeup, hair dressing and manicure (nails beauty)
———————————- ———————————-
Sahihi Tarehe
(Kwa matumizi ya ofisi)
Jina la mpokeaji form ( Mkuu wa chuo)au kwa niaba
Jina ——————————————————— Sahihi —————————— Tarehe ……………